AMBANI AWEKA IMANI KWA AFC LEOPARDS KUBEBA UBINGWA
Kocha wa AFC Leopards Fred Ambani ameendelea kuamini uwezo wa timu yake kuwania ubingwa wa Ligi kuu humu nchini licha ya kupoteza bao moja bila dhidi ya Posta Rangers katika mchezo wa maandalizi
Ambani amesema matokeo mazuri waliyopata katika mechi nyingine za maandalizi yameongeza morali kambini, baada ya Ingwe kuibuka na ushindi dhidi ya Pamba Jiji, Kakamega Homeboyz, Nairobi United, Moi Kabarak University na Kipchimchim FC
Ingwe pia ilifanya maandalizi nchini Tanzania na Uganda, huku Ambani akisema mechi hizo zimesaidia benchi la ufundi kutambua nguvu za kikosi pamoja na maeneo yanayohitaji maboresho kabla ya msimu mpya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































