#Local News

NDINDI NYORO AJITOSA KINYANG’ANYIRO CHA URAIS 2027

Kinara wa People’s Party of Kenya Ndindi Nyoro amesema yuko tayari kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027, akisema anaamini ana uwezo wa kuongoza nchi.

Mbunge huyo wa Kiharu amesema yuko tayari kupewa nafasi ya kuongoza upinzani katika kinyang’anyiro dhidi ya Rais William Ruto, akisisitiza kuwa amejitayarisha kwa jukumu hilo.

Nyoro amesema maandalizi yake yametokana na juhudi za kuelewa changamoto zinazoikabili Kenya na kutafuta suluhu ambazo anaweza kuzitekeleza iwapo atapewa nafasi ya kuongoza serikali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *