#Local News

WAUGUZI WASITISHA MGOMO BAADA YA MAKUBALIANO NA MAGAVANA

Wauguzi nchini wamesitisha mgomo wao wa wiki tano baada ya kufikia makubaliano ya kurejea kazini na Baraza la Magavana, huku pande hizo zikiahidi kutatua masuala yaliyosababisha mzozo huo.

Makubaliano hayo yanajumuisha malipo ya marupurupu ya hatari na sare yatakayoanza kuhesabiwa kuanzia Julai mosi 2025, huku serikali za kaunti zikijitolea kushughulikia malalamiko mengine yaliyosalia.

Pande hizo zimekubaliana kutatua masuala yote yaliyosalia ndani ya siku 45, hatua iliyofikiwa siku chache baada ya madaktari kutishia kugoma iwapo mgomo wa wauguzi ungeendelea na kuongeza mzigo kwa wahudumu wengine wa afya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *