MAHAKAMA YA NAIROBI IMEWAPA MAAFISA WA DCI SIKU NNE KUWASHIKILIA WASHUKIWA WAWILI WA DR VICTORIA
Mahakama ya Nairobi imewapa maafisa wa DCI siku nne zaidi kuwashikilia washukiwa wawili, Daniel Mwangi na Kevin Kinuthia, huku uchunguzi wa mauaji ya Dkt. Victoria Mutiso ukiendelea.
DCI ilikuwa imeomba siku saba zaidi ili kukamilisha uchunguzi, ikisema imepata taarifa mpya kutoka kwa washukiwa na watu wengine waliokamatwa.
Mahakama imesema washukiwa hao wazuiliwe kwa siku nne pekee, huku polisi wakisubiri ripoti za uchunguzi wa kisayansi na fedha, pamoja na kuwasaka mashahidi wengine.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































