KCB YAILAZA KABRAS KUTWAA TAJI LA EMBU 7S
KCB imeibuka mabingwa wa Embu 7s baada ya kuilaza mpinzani wake Kabras Sugar 7s kwa alama 12 kwa 10 katika fainali ya Kombe, na kutwaa taji katika awamu ya sita ya mzunguko wa kitaifa wa mwaka huu
Ushindi huo umeipa KCB nafasi nzuri zaidi katika msimamo wa jumla wa mfululizo, huku ikiwa ni mara ya tatu ndani ya awamu tano msimu huu kwa KCB na Kabras kukutana katika fainali ya Kombe
KCB imeendelea kutawala mikutano hiyo muhimu baada ya kuishinda Kabras tena, huku Embu 7s ikiwa ni awamu ya pili kutoka mwisho katika mzunguko wa National 7s Circuit wa 2026.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































