#Football #Sports

MCTOMINAY KUKOSA MECHI KADHAA KWA TATIZO LA MOYO

Kiungo wa Napoli na timu ya taifa ya Scotland Scott McTominay atakosekana hadi baada ya mapumziko ya kimataifa mwishoni mwa mwezi kutokana na tatizo dogo la mpigo wa moyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akisumbuliwa na hitilafu ya mpigo wa moyo, hali ambayo Napoli imesema si ya kutisha lakini inahitaji kufanyiwa upasuaji.

McTominay atakosa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal wiki ijayo pamoja na michezo ijayo ya Scotland dhidi ya Slovenia, Uswisi na Macedonia Kaskazini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *