STRATHMORE LEOS YALENGA KUREJESHA TAJI LA EMBU SEVENS
Nahodha Gabriel Ayimba anaamini Strathmore Leos iko tayari kurejea kwa nguvu baada ya matokeo mabaya ya Driftwood Sevens, huku ikilenga kutwaa Embu Sevens kwa mara ya tano mfululizo.
Leos ilimaliza nafasi ya 14 Mombasa ikiwa na alama mbili pekee, lakini Ayimba amesema kikosi kimejifunza kutokana na makosa hayo na kinafanya maandalizi makali kurejea katika kiwango chake.
Strathmore imetawala Embu Sevens katika misimu minne iliyopita, ikiwahi kuwashinda Menengai Oilers, Catholic Monks na KCB, huku Ayimba akiamini rekodi hiyo inaweza kuendelezwa wikendi hii.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































