#Local News

RUTO AWATAKA WAPINZANI WAACHE KELELE, WATOE MIKAKATI

Rais William Ruto amewataka wapinzani wake kuacha kile alichokiita kelele za kisiasa na badala yake kuwaeleza Wakenya wanachopanga kufanya iwapo watapewa nafasi ya kuongoza nchi.

Akizungumza Kajiado, Ruto amewataka viongozi wa upinzani kuwasilisha sera, mipango na dira zao badala ya kutumia mashambulizi ya kisiasa, akisema wananchi wanahitaji kusikia suluhu za changamoto zinazowakabili.

Rais amesema Wakenya wana uwezo wa kutofautisha viongozi wenye mipango inayotekelezeka na wale wasio na dira, hivyo kuwataka wapiga kura kuwapima viongozi kwa sera na uwezo wao wa kuleta mabadiliko.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *