ZICO AITAKA POSTA RANGERS KUMALIZA TOP FIVE
Kocha wa Posta Rangers Zedekiah “Zico” Otieno amekipa changamoto kikosi chake kipya kuhakikisha kinamaliza katika nafasi tano za juu msimu wa 2026/27 baada ya timu hiyo kunusurika kushuka daraja msimu uliopita.
Posta Rangers ilimaliza nafasi ya 15 ikiwa na pointi 40 baada ya mechi 34, jambo lililomfanya Zico kufanya mabadiliko makubwa na kuwasajili zaidi ya wachezaji kumi na wawili katika kipindi cha mapumziko.
Kocha huyo amesema maandalizi ya msimu huu yamekuwa bora zaidi kwa kuwa amepata muda wa kutosha kukijenga kikosi na kukifundisha mbinu zake, akilenga kuona Posta Rangers ikiwa imara zaidi na yenye uwezo wa kushambulia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































