MOTO WATEKETEZA MADUKA SOUTH B, NAIROBI
Moto mkubwa umezuka katika maduka yaliyoko kando ya Barabara ya Kapiti eneo la South B jijini Nairobi, huku ripoti zikisema moto huo umeanea hadi makazi ya Golden Gate Estate.
Moto huo ulianza mwendo wa saa sita usiku wa kuamkia Jumatatu na kuendelea hadi saa za mapema asubuhi, huku video zikionyesha moshi mzito na miali mikubwa ikipanda kutoka kwenye majengo ya eneo hilo.
Chanzo cha moto huo pamoja na ukubwa wa hasara bado hakijafahamika, huku juhudi za kudhibiti moto huo zikiendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































