MALKIA STRIKERS YAKATA TIKITI YA NUSU FAINALI
Malkia Strikers imefuzu nusu fainali ya Mashindano ya Afrika ya Mpira wa Wavu kwa Wanawake baada ya kuichapa Algeria kwa seti 3-1 katika robo fainali iliyochezwa Kasarani.
Algeria ilianza kwa kishindo na kushinda seti ya kwanza kwa alama 25-21, lakini Malkia Strikers ilirejea kwa nguvu mbele ya mashabiki wa nyumbani na kushinda seti tatu zilizofuata.
Mabingwa hao watetezi sasa watakutana na Cameroon katika nusu fainali Alhamisi, baada ya Cameroon kuichapa Uganda kwa seti 3-0 na kutinga hatua hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































