#Football #Sports

ENZO FERNANDEZ: SIKUSITA WAKATI MAN CITY ILIPONIITA

Kiungo wa Argentina Enzo Fernandez amesema hakusita hata kwa sekunde moja baada ya Manchester City kuwasiliana naye, kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Chelsea kwa ada ya rekodi ya pauni milioni 125.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na City siku ya mwisho ya dirisha la usajili, huku matumizi ya klabu hiyo yakifikia zaidi ya pauni milioni 450 katika dirisha moja, rekodi mpya katika Ligi Kuu ya England.

Fernandez alijiunga na Chelsea kutoka Benfica mwaka 2023 kwa pauni milioni 107, na sasa uhamisho wake kwenda City umeifikisha ada hiyo kwenye kiwango sawa na ile ya Liverpool kumsajili Alexander Isak mwaka uliopita.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

ENZO FERNANDEZ: SIKUSITA WAKATI MAN CITY ILIPONIITA

YEGO NA SEREM WATAFUTA TAJI LAO LA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *