MGOMO WA WAUGUZI WAENDELEA LICHA YA MAZUNGUMZO NA MAGAVANA
Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi na Wakunga unasema mazungumzo na Baraza la Magavana yanaendelea, lakini mgomo bado upo baada ya pande hizo kushindwa kufikia mwafaka.
Katibu Mkuu Seth Panyako anasisitiza kutekelezwa kwa Mkataba wa Makubaliano wa mwaka 2017, huku magavana wakipinga wakisema ulifikiwa chini ya shinikizo na hauwezi kutekelezwa.
Mvutano huo unaendelea hata baada ya Naibu Rais Kithure Kindiki kuagiza Wizara ya Afya kuwakutanisha wauguzi na magavana, ili kutafuta suluhu ya mgomo unaoathiri huduma za afya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































