#Local News

POLISI WALIOSIMAMIA UONDOAJI WA WATU KWENYE SHAMBA LA UTATA MLOLONGO WANAKABILIWA NA MASHTAKA

Maafisa kadhaa wa polisi waliokuwa wakisimamia uondoaji wa watu katika shamba lenye utata huko Mlolongo wanakabiliwa na mashtaka.

Uchunguzi umehusisha uondoaji huo na matukio yaliyofuata hadi kuuawa kwa daktari wa magonjwa ya akili, Victoria Nthunya Mutiso.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DCI, imependekeza polisi hao pamoja na maafisa wa mnada walioshiriki katika zoezi hilo wafunguliwe mashtaka.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *