#Rugby #Sports

KCB YAKOSA NYOTA WATANO KUELEKEA CHRISTIE SEVENS

KCB RFC itaingia katika hatua ya mwisho Ubingwa wa Kitaifa na Mahindano ya Christie Sevens jijini Nairobi wikendi hii bila nyota wake watano muhimu.

Nahodha Vincent Onyala, George Oroo, Festus Shiasi, Nigel Amaitsa na Samuel Asati wataelekea Wales kushiriki michuano ya kwanza ya Ultimate Sevens Championship jijini Cardiff Jumamosi.

Hata hivyo, kocha Andrew Amonde anapata nafasi ya kuwapa wachezaji wa kikosi cha pili majukumu makubwa katika harakati za KCB kutetea ubingwa wa Christie Sevens na National Sevens Circuit.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *