MALKIA STRIKERS YALENGA FAINALI BAADA YA KUIZIMA ALGERIA
Kocha wa Malkia Strikers Geoffrey Omondi anaamini Kenya ina uwezo wa kuishinda Cameroon na kufuzu kwa fainali ya Mashindano ya Afrika ya Mpira wa Wavu, huku mabingwa hao watetezi wakikaribia hatua ya mwisho ya kutetea taji.
Omondi amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kukabiliana na Cameroon, akitambua kuwa watakutana na upinzani mkali, huku akiwataka wachezaji kudumisha nidhamu na kutumia mafunzo waliyojifunza katika michezo iliyopita.
Kenya ilitinga nusu fainali baada ya kuishinda Algeria kwa seti 3-1 katika robo fainali, licha ya kupoteza seti ya kwanza kwa 25-21, kabla ya kushinda seti tatu zilizofuata na sasa inalenga kuendeleza ubabe wake dhidi ya Cameroon.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































