#Football #Sports

ABONDO AREJEA GOR MAHIA KUINOA TIMU YA WANAWAKE

Ali ‘Teargas’ Abondo, aliyewahi kuwa kiungo wa Gor Mahia, amerejea katika klabu hiyo akiteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Gor Mahia Queens, baada ya kuondoka kwa Tom Odiyo mwishoni mwa wiki

Gor Mahia imemtangaza Abondo kama kocha mpya wa Queens, huku kurejea kwake kukizua kumbukumbu za enzi zake uwanjani ambapo alipata umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki wa K’Ogalo

Abondo alipewa jina la utani ‘Teargas’ baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi ya Mashemeji Derby mwaka 2012, tukio lililochochea vurugu na mapambano kati ya polisi na mashabiki baada ya mchezo huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *