#Rugby #Sports

CHRISTIE 7S KUAMUA NANI BINGWA KATI YA KCB NA KABRAS

KCB na Kabras zitachuana kuwania ubingwa wa National Sevens Circuit ya 2026 katika mashindano ya  Christie 7s, ikiwa ni hatua ya mwisho ya msimu itakayofanyika uwanja wa RFUEA Grounds wikendi hii.

KCB inaongoza msimamo kwa alama 98, ikifuatiwa na Kabras yenye alama 92, huku Menengai Oilers ikiwa ya tatu kwa alama 75, Daystar Falcons 67 na Kenya Harlequins 64.

KCB imeshinda hatua tatu kati ya tano zilizochezwa hadi sasa, huku Kabras ikitwaa hatua mbili, hivyo Christie 7s inatarajiwa kuamua bingwa wa msimu huu katika pambano kali kati ya vinara hao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *