#Local News

LINDA MWANANCHI KUTANGAZA CHAMA KIPYA OKTOBA

Kikosi cha Linda Mwananchi katika eneo la Magharibi mwa Kenya kimetangaza mipango ya kuzindua chama kipya cha kisiasa tarehe moja Oktoba, kikisema chama hicho kitakuwa jukwaa la Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwania urais mwaka 2027.

Kikosi hicho kimesema hatua hiyo inalenga kumpa Sifuna nafasi ya kuendeleza azma yake ya kisiasa na kujenga uungwaji mkono nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Tangazo hilo linajiri huku shughuli za kisiasa zikizidi kushika kasi, na makundi mbalimbali ya upinzani yakijipanga na kuunda miungano kuelekea uchaguzi wa 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *