SIFUNA AMEMKARIBISHA MUKHISA KITUYI KWENYE SIASA ZA LINDAMWANANCHI
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amemkaribisha aliyekuwa Waziri wa Biashara Mukhisa Kituyi katika harakati za kisiasa za Linda Mwananchi.
Kituyi alitembelea ofisi ya Sifuna Jumatano asubuhi, akiwa ameandamana na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi.
Sifuna amesema Kituyi ni nyongeza muhimu kwa vuguvugu hilo linaloungwa mkono na upinzani, huku likijiandaa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































