IEBC YAONYA JUU YA KUONGEZEKA KWA VURUGU ZA UCHAGUZI
Wadau wa uchaguzi wameonya kuhusu kuongezeka kwa visa vya vurugu za kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, wakisema hali hiyo inatia wasiwasi.
Katika mkutano wa usalama na IEBC jijini Nairobi, wadau wametaja Homa Bay, Nakuru, Bomet na Migori, wakisema mwenendo huo unafanana na hali iliyotangulia ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 na 2008.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema takriban maafisa 200,000 wa polisi wanaendelea na mafunzo kuelekea uchaguzi huo, katika juhudi za kuimarisha usalama na amani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































