#Local News

WANAHARAKATI KUFANYA MAANDAMANO KUPINGA KUTEKWA KWA BESIGYE

Wanaharakati nchini Kenya wamepanga kufanya maandamano ya kitaifa Alhamisi Septemba 3, wakitaka majibu kuhusu madai ya kutekwa na kusafirishwa kinyume cha sheria kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye.

Kesi ya Besigye imezua wito wa uwajibikaji katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, huku maswali yakiongezeka kuhusu namna alivyoshughulikiwa na mamlaka.

Wakati huohuo, hali yake ya kiafya inatajwa kuwa inazidi kuwa mbaya, jambo ambalo limeongeza shinikizo kwa serikali za eneo hilo kutoa ufafanuzi na kuhakikisha haki zake zinalindwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *