#Local News

MUKHISA KITUYI : AMRI YA RUTO KWA WAGENI INATISHIA USALAMA WA WAKENYA.

Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mukhisa Kituyi amemuonya Rais William Ruto kuwa agizo dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni nchini linaweza kuwaweka Wakenya wanaoishi na kufanya kazi katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki hatarini.

Kituyi amesema kulenga wafanyabiashara wa kigeni kwa ujumla kunaweza kuzua mvutano wa kikanda, akimtaka serikali kudhibiti biashara zao kwa kuzingatia sheria bila kuhusisha utaifa na siasa.

Kauli hiyo inajiri baada ya Rais Ruto kuagiza hatua dhidi ya wageni wanaojihusisha na biashara ndogo na biashara zisizo rasmi, akisema baadhi ya shughuli hizo zinapaswa kuhifadhiwa kwa raia wa Kenya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *