#Football #Sports

MAN UNITED YAPANGA MKATABA MPYA NA KOBBIE MAINOO

Klabu ya Manchester United imepanga kuzungumza kuhusu mkataba wa muda mrefu na kiungo wake Kobbie Mainoo, baada ya kuonyesha mchango mzuri chini ya kocha Michael Carrick.

Mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 2027, ukiwemo chaguo la kuongeza msimu mmoja hadi 2028, lakini United wanataka kuanza mazungumzo ya mkataba mpya mapema mwaka huu ili kumhakikishia huduma ya Mainoo kwa muda mrefu.

United imedokeza kuwa wanaridhishwa na maendeleo yake kikosini na wanasema mchakato wa mazungumzo utahakikisha mchezaji huyo anabaki kuwa sehemu ya timu kuu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

MAN UNITED YAPANGA MKATABA MPYA NA KOBBIE MAINOO

ALDRINE KIBET ANG’ARA HISPANIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *