#Football #Sports

KENYA KUWA MWENYEJI WA FIFA SERIES APRILI

Kenya itakuwa mwenyeji wa mojawapo ya makala ya FIFA Series kitengo cha wanawake, yatakayoandaliwa nchini mwezi ujao.

Mashindano hayo yatajumuisha wenyeji Harambee Starlets, Australia, Malawi na India.

Kenya itashuka dimbani katika mechi ya pili dhidi ya India baada ya Malawi kumenyana na Australia, mechi zote zikiratibiwa kuchezwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Kulingana na maafisa wakuu katika sekta ya michezo akiwemo Waziri wa michezo Salim Mvurya na rais wa FKF Hussein Mohammed, mechi hizo ni za kirafiki na wala si za kufuzu katika mashindano ya kombe lolote.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *