MAHAKAMA YAONGEZA AMRI KUHUSU MCHAKATO WA KUMWONDOA DPP
Mahakama Kuu imeongeza muda wa amri ya kusitisha mchakato wa kuandaa kanuni za kumwondoa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.(DPP)
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mahakama kuthibitisha kuwa kesi inayotaka maafisa wa Tume ya Huduma za Umma kushtakiwa kwa kudharau mahakama ni ya dharura.
Mahakama imeagiza maombi yawasilishwe kwa wahusika wote ndani ya siku tatu, huku wakijibu ndani ya siku saba, na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 9 kwa maelekezo zaidi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































