BABY PENDO: MAHAKAMA KUTOA MWELEKEO
Mahakama kuu ya Milimani jijini Nairobi imeratibiwa kutoa mwelekeo kuhusu uamuzi wa kuwaondolea mashtaka maafisa wakuu 8 wa polisi wanaohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 katika kaunti ya Kisumu ikiwemo mauaji ya mtoto Samantha Pendo maarufu kama Baby Pendo.
Katika ombi lililowasilishwa mahakamani humo, familia ya Pendo, waathiriwa wengine wa ghasia hizo na makundi ya taasisi za kiraia, yanamtaka mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga kurejesha mashtaka dhidi ya maafisa hao, wakisema uamuzi wa awali unadhoofisha upatikanaji wa haki.
Mashtaka hayo yaliwasilishwa awali kama kesi ya jinai katika mahakama kuu ya Nairobi mwaka 2022 kabla ya kuhamishiwa Kisumu mwaka jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































