MABADILIKO YAPENDEKEZWA KUHARAKISHA CHETI CHA GOOD CONDUCT
Wakenya huenda wakaanza kupata vyeti vya tabia njema kwa haraka na kwa gharama nafuu kufuatia pendekezo la marekebisho ya sheria yanayolenga kuifanya huduma hiyo kuwa ya kidijitali na kuondoa ulazima wa kuchukuliwa alama za vidole kila mara.
Kamati ya Bunge ya Usalama na Utawala imekuwa ikipitia mabadiliko ya Sheria ya Huduma ya Polisi yanayopendekeza matumizi ya taarifa za kibayometriki zilizohifadhiwa ili kurahisisha maombi ya mara kwa mara kupitia mfumo wa mtandao wa kitaifa.
Ikiidhinishwa sheria hiyo itawawezesha waombaji kutumia taarifa zilizopo badala ya kufika vituo vya huduma kama Huduma Centre au ofisi za DCI kila mara hatua inayotarajiwa kupunguza msongamano na kuboresha ufanisi wa huduma kwa umma nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































