WANAFUNZI KADHAA WAFARIKI KATIKA MOTO WA BWENI LA WASICHANA LA UTUMISHI
Moto mkubwa umezuka alfajiri katika shule ya wasichana ya Utumishi Academy eneo la Gilgil na kusababisha hofu ya vifo pamoja na majeruhi kadhaa baada ya bweni moja kuteketea kwa moto.
Ripoti za awali zinaonyesha kuwa baadhi ya wanafunzi wanahofiwa kufariki huku wengine wakijeruhiwa na wengine kuathiriwa na moshi, hali ambayo imezua taharuki kubwa miongoni mwa wanafunzi, walimu na wazazi.
Kamanda wa eneo pana la Bonde la Ufa Masoud Mwinyi amesema maafisa wanaendelea kukagua kila sehemu ya shule hiyo ili kupata taarifa kamili kuhusu tukio hilo, akieleza kuwa huzuni ya familia zilizoathirika ni jambo la kusikitisha kwa kila mmoja.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































