#Football #Sports

GOR MAHIA YAPIGWA 2-0 NA PYRAMIDS.

Gor Mahia imepata pigo katika harakati zake za kimataifa baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya miamba ya Misri Pyramids FC katika Uwanja wa Nyayo Jumapili.

Pyramids ilianza kwa kasi huku Walid El Karti akifunga bao la kwanza dakika ya tano, kabla ya Mahmoud Saber kuongeza la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kuwaacha mabingwa hao wa Kenya wakisaka majibu.

Bao la mapema liliiweka Gor Mahia katika presha kubwa, huku vijana wa Charles Akonnor wakishindwa kupata nafasi ya kubadili matokeo na sasa wakikabiliwa na kazi ngumu katika safari yao ya kusaka mafanikio barani Afrika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

GOR MAHIA YAPIGWA 2-0 NA PYRAMIDS.

ARSENAL YAILAZA CHELSEA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *