MAN CITY NA REAL MADRID WAANZA UCL KWA USHINDI
Jose Mourinho ameanza kwa ushindi kurejea katika Ligi ya Mabingwa akiwa kocha wa Real Madrid, baada ya miamba hao wa Hispania kuishinda Inter Milan kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya ligi, huku Erling Haaland akifunga mabao mawili Manchester City ilipoilaza Porto
Real Madrid ilipata mabao mawili katika kipindi cha kwanza baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Inter, huku Kylian Mbappe akifungua ukurasa wa mabao na kufikisha idadi yake ya mabao 71 katika michuano hiyo, sawa na rekodi ya gwiji wa Madrid Raul
Mourinho amerejea Madrid kwa mara ya pili na mchezo huo ukawa wa kipekee kwake kwani Inter ndiyo timu aliyoiwezesha kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2010, Wakati huohuo Aston Villa na Borussia Dortmund pia zilianza msimu kwa ushindi katika michezo mingine.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































