#Football #Sports

SELEBWA : KENYA INAWEZA KUFUZU AFCON U-20

Kocha wa Rising Stars Gilbert Selebwa anaamini kikosi chake kina uwezo wa kuiwezesha Kenya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Afrika kwa wachezaji walio chini ya miaka 20 mwaka 2027 nchini Ghana kupitia michuano ya kufuzu ya CECAFA nchini Tanzania.

Selebwa ametangaza kikosi cha mwisho kilichochanganya vipaji kutoka shule pamoja na wachezaji wa vilabu vya ndani na nje ya nchi, huku wanne pekee Telena Ochieng, Humphrey Okoth, Raphael Omondi na Austin Odongo wakinusurika kutoka kikosi cha awali cha wachezaji 64.

Kikosi hicho pia kina wachezaji waliopanda kutoka timu ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17 ya mwaka jana, akiwemo Omondi, Trevor Nasasiro, Yusuf Ahmed, Armstrong Omondi pamoja na watatu kutoka Shule ya Kakamega Eugine Belety, Brighton Nacheri na Julius Ochieng.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *