#Football #Sports

ODEGAARD AIPA ARSENAL USHINDI WA KWANZA ULAYA

Nahodha wa Arsenal Martin Odegaard ameifungia timu yake bao la ushindi dakika za mwisho na kuipa ushindi wa bao moja bila dhidi ya Napoli katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa mjini Naples Jumatano.

Arsenal ilipoteza nafasi kadhaa za wazi dhidi ya Napoli iliyocheza kwa nidhamu, kabla ya Odegaard kupiga shuti kutoka nje ya eneo la hatari lililogonga mwamba na kuingia wavuni, huku bao hilo likija zikiwa zimesalia dakika 15.

Ushindi huo unaendeleza mwanzo bora wa Arsenal msimu huu, baada ya kuanza kampeni ya Ligi Kuu kwa ushindi wa mechi tatu mfululizo, huku Napoli ikipata kichapo chake cha tatu mfululizo katika michuano yote.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *