EACC YAMKAMATA ALIYEKUWA DCIO WA LIKONI KWA TUHUMA ZA UFISADI
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemkamata aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai wa Wilaya ya Likoni (DCIO), Charles Onyango KA’galo.
Msemaji wa EACC, Eric Ngumbi, amesema kuwa KA’galo amekamatwa katika nyumba yake ya kijijini huko Oyugis. Na kwamba anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Port akisubiri kufikishwa mahakamani.
Ngumbi amesisitiza kuwa EACC imejizatiti kupambana na ufisadi katika ngazi zote za utumishi wa umma.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































