WAATHIRIWA WA JANGA LA BWAWA LA MAI MAHIU WAKABILIWA NA CHANGAMOTO MPYA
Waathiriwa wa maafa ya bwawa la Mai Mahiu, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 60, wamepata pigo jipya baada ya serikali kuzuia mashirika mawili ya hisani kujenga nyumba 14 kwa familia zilizoathirika.
Serikali na wamiliki wa ardhi wanadaiwa kutofautiana kuhusu gharama ya ardhi, jambo lililokwamisha mpango wa makazi ya KSh. milioni 250.
Mashirika hayo yameagizwa kupata kibali kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kabla ya kuanza ujenzi.
Baadhi ya waathiriwa, wameeleza machungu yao, wakishangaa kwa nini serikali inazuia misaada huku wakihangaika bila makazi.
Ujenzi huo unadaiwa kusitishwa hadi tathmini ifanywe katika eneo lililoathirika.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































