#Local News

WAJACKOYAH AFICHUA KWA NINI YUKO NJE YA UNITED OPPOSITION

Kiongozi wa Roots Party George Wajackoyah amesema hajajiunga na Muungano wa Upinzani kwa sababu viongozi wa muungano huo hawajawahi kumwalika, huku vyama vya kisiasa vikijipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027

Wajackoyah amesema bado ana mawasiliano na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka licha ya kutokuwa mwanachama wa Muungano wa Upinzani, akisema wawili hao huwasiliana na wakati mwingine kukutana

Hata hivyo, Wajackoyah amesema uamuzi wake wa kubaki nje ya Muungano wa  upinzani pia ulitokana na kile anachokiona kuwa ukosefu wa mpango wazi wa sera kwa nchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *