MATHARE UNITED YAFANYA USAJILI WA WACHEZAJI 13 KABLA YA MSIMU MPYA
Mathare United imefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kuelekea msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu nchini, huku kocha David Ouma akitumia dirisha la usajili kurekebisha udhaifu uliochangia timu hiyo kusuasua msimu uliopita.
Slum Boys imesajili wachezaji 13 akiwemo Michael Kyalo, Christopher Oruchum, Joshua Nyatini, Simon Masaka, Kent Wanyama na Victor Omune.
Mathare ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya 14 kwa alama 41 baada ya mechi 34, huku Ouma aliyerejea klabuni mwezi Juni akilenga kuimarisha safu ya ulinzi na ushambuliaji baada ya maeneo hayo kuonyesha udhaifu katika mechi za maandalizi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































