#Local News

WABUNGE WATILIA SHAKA UFANISI WA MFUMO WA UNUNUZI WA SERIKALI

Kamati ya Bajeti na Matumizi ya Bunge imehoji ufanisi wa mfumo wa kielektroniki wa ununuzi ya serikali baada ya kubaini kuwa serikali za kitaifa na kaunti zinaendelea kukusanya madeni ya malipo yaliyochelewa licha ya mageuzi hayo.

Maafisa wa Hazina ya Kitaifa waliambia kamati kuwa taasisi 1,546 za ununuzi zilikuwa zimesajiliwa katika mfumo wa ununuzi ya serikali kwa njia ya kielektroniki kufikia Juni 2026, karibu mwaka mmoja baada ya kuanzishwa rasmi Julai mosi 2025.

Hata hivyo, wabunge wametaka ushahidi wa wazi kuwa mfumo huo unatimiza lengo la kuongeza ufanisi, uwazi na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma, hasa wakati ambapo malimbikizo ya madeni ya serikali yanaendelea kuongezeka.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *