#Rugby #Sports

SHUJAA NA LIONESSES ZAPATA NAFASI TATU ZA KUFUZU OLYMPIC 2028

Shujaa na Kenya Lionesses zimepata nafasi tatu za kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles 2028 baada ya shirikisho la Raga Duniani kuthibitisha mfumo wa kufuzu, huku mbio hizo zikianza katika msimu wa HSBC SVNS 2027.

Njia ya moja kwa moja kwa Kenya ni kumaliza katika timu nne bora zinazostahiki kufuzu katika msimamo wa SVNS 2027 kwa wanaume na wanawake, isipokuwa Marekani ambayo itafuzu moja kwa moja kama mwenyeji.

Hivyo Shujaa na Lionesses watalazimika kukusanya alama za kutosha katika mashindano yote ya msimu wa 2027 ili kumaliza ndani ya nne bora, huku kila hatua ikiwa muhimu katika safari yao kuelekea Los Angeles.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *