#Local News

OMTATAH AFUNGIWA VIKAO VITATU SENETI KWA KUMKOSOA RUTO

Seneta wa Busia Okiya Omtatah amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo vya Seneti baada ya kukataa kuondoa na kuomba msamaha kwa kumtaja Rais William Ruto kuwa anatoa kauli zisizo na msingi.

Spika wa Seneti Amason Kingi alimuamuru Omtatah kuondoka ukumbini baada ya seneta huyo kupinga agizo la kuondoa matamshi yake, akisisitiza kuwa neno alilotumia halikuwa kinyume na kanuni za Bunge.

Mzozo huo ulizuka katika kikao cha Jumatano mchana wakati Omtatah akizungumzia kauli za Ruto kuhusu kufungwa kwa biashara ndogo zinazoendeshwa na wageni pamoja na kampuni ya Tata, ambapo Spika alisema matamshi hayo hayafai kutumiwa ndani ya Seneti.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *