#Local News

RUTO AWAPA UPINZANI MASHARTI KABLA YA UCHAGUZI WA 2027

Rais William Ruto amesema serikali yake imetekeleza ajenda yake ya maendeleo na kuwataka viongozi wa upinzani kuwasilisha sera mbadala zilizo wazi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Ruto amewakosoa viongozi hao kwa kujikita katika mipango ya kumuondoa madarakani badala ya kutoa suluhu za gharama ya maisha na ukosefu wa ajira unaowakabili Wakenya.

Rais amesema kumshinda katika uchaguzi ujao kutakuwa changamoto kubwa kwa upinzani kutokana na kile alichokitaja kuwa ukosefu wa ilani ya kisiasa yenye mwelekeo na sera mbadala zinazoaminika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *