KENYA YAIMARISHA UKAGUZI WA EBOLA MPAKANI
Serikali ya Kenya imeimarisha uangalizi na ukaguzi katika mpaka wa Busia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo uliosababisha zaidi ya vifo 130.
Serikali imetuma timu ya wahudumu wa afya kuwachunguza wasafiri wanaotoka ukanda wa Maziwa Makuu baada ya taarifa kuwa nchi jirani ya Uganda tayari imeripoti kifo kimoja kinachohusishwa na virusi vya Ebola.
Maafisa wa afya kaunti ya Busia wakiongozwa na Waziri wa Afya wa kaunti hiyo Arthur Odera wamesema hatua hizo zinalenga kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo nchini kupitia mipaka ya kimataifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































