#uncategorized

KENYA YATARAJIWA KUPOKEA SHILINGI BILIONI 52 FEDHA ZA DHARURA KUTOKA BENKI YA DUNIA

Kenya inatarajiwa kupokea takriban shilingi bilioni 52 sawa na dola milioni 400 kama fedha za dharura kutoka Benki ya Dunia ndani ya wiki sita, ili kusaidia kulinda uchumi dhidi ya hatari zinazohusiana na Ebola, athari za El Niño, na bei ya juu ya nishati.

Ripoti zimenukuu chanzo chenye taarifa za ndani kuhusu suala hilo, na kuashiria kuwa Kenya iliomba kutumia utaratibu wa Benki ya Dunia wa ‘Rapid Response Option’ (Mpango wa Majibu ya Haraka) baada ya mzozo wa Iran kusababisha kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta ghafi duniani.

Fedha hizo zinatarajiwa kusaidia sekta ya afya, kilimo, rasilimali za maji, na uthabiti wa jumla wa uchumi.Benki ya Dunia imethibitisha kuwa inashirikiana na Kenya kukamilisha mfumo utakaowezesha upatikanaji wa haraka wa fedha wakati wa majanga yanayostahiki msaada huo. Kwa sasa, Kenya ina miradi ya Benki ya Dunia yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 910.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

KENYA YATARAJIWA KUPOKEA SHILINGI BILIONI 52 FEDHA ZA DHARURA KUTOKA BENKI YA DUNIA

MAN UNITED YADHALILISHA SABAH 4-0

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *