MBUNGE WA SOTIK AMUOMBA RAIS MSAMAHA KWA KUSEMA WANTAM
Mbunge wa Sotik, Francis Sigei, amemuomba msamaha Rais William Ruto baada ya kauli aliyoitoa katika mkutano wa kisiasa mjini Bomet kutafsiriwa kama kuunga mkono kaulimbiu ya upinzani ya ‘WANTAM’.
Sigei amesema alikusudia kumhimiza Rais Ruto kuhudumu kwa muhula mmoja zaidi, na wala si muhula mmoja pekee kama kauli yake ilivyoweza kueleweka.
Mbunge huyo amesema tayari amemuomba Rais msamaha na kufafanua kuwa matamshi yake yalisababisha mkanganyiko.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































