IDADI YA WAFANYAKAZI VYUONI KUPUNGUZWA
Mamia ya wafanyakazi katika vyuo vikuu vya umma nchini wanakabiliwa na hatari ya kuachwa bila ajira baada ya serikali kutangaza kwamba haina uwezo wa kufadhili elimu katika vyuo hivyo.
Waziri wa fedha John Mbadi ametangaza kwamba serikali imeweka mpango wa kuvinusuru vyuo hivyo, ikiwemo kufunga baadhi ya mabewa na kupunguza idadi ya wafanyakazi ili kudhibiti mzigo wa fedha.
Tangazo la serikali kwamba haina fedha linakuja wakati ambapo vingi vya vyuo vinakabiliwa na madeni na changamoto za kifedha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































