MACHO EAC KUHUSU MZOZO WA KENYA-TANZANIA
Macho yote sasa yameelekezwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashiriki EAC kuona ni hatua zipi zitakazochukuliwa ili kuzima mzozo wa kidiplomasia uanotokota kati ya Kenya na Tanzania.
Hii ni baada ya Kenya kuiandikia rasmi Jumuiya hiyo kupinga vikwazo vya kibiashara vilivyowekwa na Tanzania kuhusu kufanya biashara nchini humo, katibu mkuu katika idara ya EAC Caroline Karugu, akisema vikwazo hivyo vinakiuka itifaki za soko la pamoja la EAC.
Miongoni mwa itifaki hizo ni uhuru wa raia wa jumuiya hiyo kusafiri, kuhudumu na haki ya kuanzisha biashara katika mataifa wanachama.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































