KDF YABAINISHA WALIOUAWA LAMU
Watu 5 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab waliouawa hapo jana katika msitu wa Boni kaunti ya Lamu walikuwa wakipanga njama ya kuteka kituo cha usalama kilicho eneo hilo.
Haya yamebainishwa na idara ya jeshi la ulinzi KDF, ambayo imesema maafisa wake waligundua na kusambaratisha kambi ya muda ya kundi hilo na kuwaua 5 hao ila wengine wakatoroka na majeraha.
Kupitia taarifa rasmi, KDF imewataka wakazi kuwa waangalifu licha ya keshi kutibua shambulio la kigaidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































