#Boxing #Sports

OKAKA ASIFIA MPANGO WA NDONDI MASHINANI BAADA YA KENYAKUNG’ARA DUBAI

Bondia wa Kenya Defence Forces Robert Okaka ameusifu mpango wa Ndondi Mashinani
kwa mchango wake mkubwa katika mafanikio ya timu ya taifa ya ndondi katika Mashindano
ya Dunia ya Elite World Boxing Championships) yaliyofanyika Dubai, akielezea kiwango
cha jumla kuwa cha kuridhisha zaidi ya wastani.

Mpango huo wa kukuza vipaji mashinani ulioanzishwa mwaka 2019 umeelezwa kuwa nguzo
muhimu iliyoiwezesha Hit Squad kuonyesha kiwango bora zaidi katika mashindano ya dunia
kwa zaidi ya miaka 40.

Nchini Dubai, Kenya ilishinda mapambano matano, tofauti na matoleo ya awali ambapo mara
nyingi timu ilikuwa ikitolewa mapema. Bondia wa uzani wa bantam Shaffi Bakari,
featherweight Paul Omondi, lightweight Washington Wandera na light heavyweight Robert
Okaka walionyesha dalili njema na matumaini makubwa katika jukwaa la dunia.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

OKAKA ASIFIA MPANGO WA NDONDI MASHINANI BAADA YA KENYAKUNG’ARA DUBAI

KCB RFC YALENGA KOMBE LA ENTERPRISE CHINI

OKAKA ASIFIA MPANGO WA NDONDI MASHINANI BAADA YA KENYAKUNG’ARA DUBAI

AMBANI AONA NAFASI YA UBINGWA BAADA YA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *