#Football #Sports

KPL: AMBANI AAMINI AFC LEOPARDS TAYARI KUPIGANIA UBINGWA WA LIGI

Kocha mkuu wa AFC Leopards, Fred Ambani, amesema ana imani kubwa kuwa kikosi chake kiko tayari kutoa ushindani wa kweli katika mbio za kutwaa taji la Ligi Kuu ya Kenya, KPL, msimu huu.

Ambani, ambaye alikuwa miongoni mwa kikosi kilichotwaa ubingwa wa mwisho wa ligi wa klabu hiyo mwaka 1998 pamoja na ndugu yake na mwenyekiti wa sasa wa klabu Boniface Ambani, anaamini huu ni wakati mwafaka wa kukomesha ukame wa miaka 27 bila taji la ligi.

Leopards waliimarisha azma yao ya ubingwa baada ya ushindi mnono wa mabao 4–0 dhidi ya Tusker FC katika Uwanja wa Nyayo Jumapili, ushindi uliokuwa wa nane kwao msimu huu.

Baada ya mechi 16, mabingwa hao mara 12 wamevuna pointi 30, 3 mbele ya wapinzani wao wakubwa Gor Mahia, baada ya kushinda mechi 8, sare 6 na kupoteza 2.

AFC Leopards watarejea dimbani Jumamosi dhidi ya APS Bomet kabla ya kuwakaribisha Nairobi United tarehe 25 Januari, huku duru ya pili ya msimu ikianza.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KPL: AMBANI AAMINI AFC LEOPARDS TAYARI KUPIGANIA UBINGWA WA LIGI

OGAMBA AONYA DHIDI YA SIASA SHULENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *