WANAWE ODINGA WAINGILIA MGOGORO ODM
Mgogoro kuhusu uongozi wa ODM umechukua mkondo tofauti, wanawe kinara mwanzilishi wa chama hicho Raila Odinga, Winnie Odinga na Raila Odinga Junior wakiingilia mgogoro huo na kuwatuhumu baadhi ya viongozi kwa kulenga kuwahangaisha viongozi wachanga chamani.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara, wawili hao wameshinikiza kuandaliwa kwa kongamano la kitaifa, NDC, kabla ya mazungumzo ya ushirikiano wa kisiasa na UDA ambako pia wanalenga kuwasilisha malalamishi yao.
Migawanyiko zaidi imeshuhudiwa wakati gavana wa Kakamega Fernandez Barasa na mtangulizi wake Wycliffe Oparanya wakiandaa mikutano miwili ya ODM kwenye kaunti hiyo, kinara Oburu Oginga akilazimika kuhudhuria yote.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































